Responsive image
Responsive image
Posted : March 24, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, Joseph Simbakalia.
Responsive image

Mamlaka ya maeneo maalumu ya uwezekazaji –EPZA- imewaomba mabalozi wapya wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi tano za Afrika na mashariki ya kati kuwatafuta wawekezaji wanaoweza kuanzisha viwanda hapa nchini.

 

Mkurugenzi mkuu wa EPZA Joseph Simbakalia amewaambia mabalozi hao walipotembelea kituo cha uwekezaji cha Benjamini Mkapa kilichopo Mabibo External jijini Dar es salaam kuwa wanahitaji viwanda katika maeneo hayo ili kutengeneza bidhaa zitakazouzwa nje ya nchi na kuongeza pato la taifa.

 

Baadhi ya mabalozi hao Grace Mgovano anayekwenda Uganda na Dakta Pindi Chana anayekwanda Kenya wamesema wamejionea viwanda vya nguo vinavyozalisha bidhaa zenye ubora wa juu zinazouzwa nchini Marekani na Ulaya ambazo hazina tofauti na zile zinazozalishwa katika nchi hizo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment