Responsive image
Responsive image
Posted : March 24, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Rais John Magufuli akitoa maagizo kuhusiana na makontena 20 ya mchanga wenye madini (yanayoonekana kwa nyuma) ambayo yamezuiliwa bandarini tangu alipopiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi mapema mwezi huu.
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini ambayo yamezuiliwa bandarini tangu alipopiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi mapema mwezi huu.

 

Rais Magufuli ameshuhudia makontena hayo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu katika bandari hiyo.

 

Baada ya kushuhudia makontena hayo Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini -IGP Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

 

Rais MAGUFULI pia ameshuhudia udanganyifu unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake limebeba magari matatu ya kifahari.

 

Katika hatua nyingine, Rais JOHN MAGUFULI amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi sita wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

 

Mabalozi waliowasilisha hati zao ni kutoka nchi za

 

Hungary, Guinea, Botswana, Niger,  Belarus  na  Mauritius.  

 

 

MACHI 23, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment