Responsive image
Responsive image
Posted : March 23, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Hali ya usalama katika mji wa Allepo nchini Syria bado ni tete.
Responsive image

Mazungumzo ya awali ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza mapigano nchini Syria yameanza tena mjini Geneva nchini Uswizi.

 

Pande kuu zinazohusika na mazungumzo hayo ikiwa ni upande wa upinzani nchini Syria na wawakilishi wa serikali ya nchi hiyo, zimekuwa na mazungumzo kabla ya kuanza rasmi kwa mazungumzo hayo ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

 

Mazungumzo rasmi ya amani nchini Syria yanatarajiwa kuanza kesho Ijumaa.

 

Pande hizo mbili hivi sasa zinajadiliana kuhusiana na ghasia pamoja na mapigano makali yanayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment