Responsive image
Responsive image
Posted : March 23, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Sehemu ya kivuko cha abiria kilichozama miaka mitatu iliyopita nchini Korea Kusini na kusababisha vifo vya zaidi ya abiria mia tatu ikionekana juu ya uso wa maji wakati juhudi za kukiopoa zikiendelea.
Responsive image

Wataalamu wa masuala ya baharini wamefanikiwa kuopoa kwa asilimia kubwa kivuko cha abiria kilichozama miaka mitatu iliyopita nchini Korea Kusini na kusababisha vifo vya zaidi ya abiria mia tatu.

 

Wataalamu wa masuala ya bahari wanasema wanalazimika kuopoa kivuko hicho ili kujua sababu ya kivuko hicho kuzama na kusababisha idadi kubwa ya vifo vya abiria.

 

Baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya kivuko hicho kabla ya kuzama, hawajapatikana hadi leo, na kumekuwa na juhudi za kukiopoa kwa matumaini kuwa huenda miili ya abiria hao ambao hawajapatikana hadi sasa ikakutwa kwenye mabaki ya kivuko hicho.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment