Responsive image
Responsive image
Posted : March 23, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Nahodha wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania, Mbwana Samatta.
Responsive image

Nahodha wa timu ya Taifa ya soka ya Tanzania, Mbwana Samatta  ameanza rasmi mazoezi ya kuajinda na mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

 

Samatta amesema mchezo huo una umuhimu mkubwa kwa Taifa Stars ingawa utakuwa  mgumu kwa timu zote mbilia lakinia wao  watambanana ili waweze kufanya vizuri katika mchezo huo.

 

Samatta anaendelea kuwa nahodha wa timu hiyo baada ya kocha mpya wa Taifa Stars, Salum Mayanga kuthibitisha kuwa mshambuliaji huyo wa Rk Gent ya Ubelgiji ataendelea na majukumu hayo huku akisaidiwa na Himid Mau (NINJA) na Jonas Mkude

 

Taifa Stars itacheza michezo miwili ya kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA ambapo Jumamosi hii itacheza na Botswana na Jumanne ijayo Machi 28 itacheza na Burundi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment