Responsive image
Responsive image
Posted : February 17, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Msuluhishi wa mgogoro wa BURUNDI, Rais Mstaafu wa TANZANIA, BENJAMIN MKAPA.
Responsive image

Mazungumzo ya kutafuta usuluhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini BURUNDI yameanza kwa mara nyingine Jijini ARUSHA chini ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu BENJAMIN MKAPA.

 

Akizungumza Jijini ARUSHA, MKAPA amesema kwa awamu hii ambapo mazungumzo hayo yatadumu kwa Siku TATU atakutana na vyama vya siasa na anaandaa utaratibu wa kuialika Serikali ya BURUNDI.

 

Mwenyekiti wa Chama cha Siasa cha FNL nchini BURUNDI, JACQUES BIGIRAMANA amesema mazungumzo hayo yanaweza kuleta maendeleo katika nchi yao na hata kama serikali haijafika katika mazungumzo hayo lakini wana imani kuwa iwapo wakifika watafanya mazungumzo ya amani.

 

Mazungumzo hayo ni mfululizo wa mikutano ambayo BENJAMIN MKAPA amekuwa akifanya na makundi mbalimbali ndani na nje ya BURUNDI katika jitihada za kutatua mgogoro wa kisiasa uliodumu kwa miaka MIWILI nchini humo.

 

 

SECHELELA KONGOLA

FEBRUARI 16, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment