Responsive image
Responsive image
Posted : February 16, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya watuhumiwa wa ugaidi, RWANDA
Responsive image

Kesi ya kwanza ya watu wanaotuhumiwa na ugaidi imeanza kusikilizwa nchini Rwanda ikiwahusisha watuhumiwa zaidi ya 50.

 

Watuhumiwa kutoka jamii ya Waislam nchini Rwanda wameshtakiwa kwa makosa ya kushirikiana na makundi ya kigaidi likiwemo kundi la Islamic State.

 

Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari nchini humo, baada ya saa kadhaa za kusoma maelezo binafsi ya kila mtuhumiwa, mwendesha mashitaka ameomba kesi kuendelea kwa faragha kwa madai kuwa ni kesi nzito na pengine inayoweza kuhatarisha usalama wa taifa ikiwa itasikilizwa hadharani.

 

Mawakili wa washitakiwa wamepinga hoja hiyo wakisema haina msingi wakati huu ambapo upelelezi dhidi ya wateja wao ulimalizika na kwamba kwa ngazi iliyofikiwa hakuna hofu yoyote ya kupoteza ushahidi ama kuhatarisha usalama wa taifa.

 

Aidha upande wa utetezi umeweka pingamizi za kwamba baadhi ya washukiwa hawajatimiza umri wa miaka 18 ambapo mahakama hiyo haina mamlaka ya kuendesha kesi dhidi yao.

 

Watu hao wamezuiliwa kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 15 mwezi ujao.

 

 

EDWARD KONDELA

FEBRUARI 16, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment