Responsive image
Responsive image
Posted : February 15, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Balaozi wa MAREKANI nchini UGANDA, DEBORAH MALAC.
Responsive image

MAREKANI  imesema itaipatia UGANDA msaada wa zaidi ya dola milioni 25 za kimarekani kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na wimbi la wakimbizi wanaokimbilia nchini humo.

 

Balaozi wa MAREKANI nchini UGANDA, DEBORAH MALAC amesema msaada huo wa kibinadamu umetolewa kutokana na  nchi hiyo kuwa na sera endelevu ya wakimbizi.

 

Msaada huo utatumika kuimarisha huduma za maji safi na maji taka katika kambi za wakimbizi, kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji wa kijinsia  na kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo kwenye kambi hizo.

 

UGANDA ina zaidi ya wakimbizi milioni moja ambapo kati ya hao laki saba wanatoka katika nchi jirani ya SUDAN Kusini.

 

 

MARTHA NGWIRA

FEBRUARI 15, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment