Responsive image
Responsive image
Posted : March 08, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Rais wa MAREKANI, DONALD TRUMP.
Responsive image

Ikulu ya KENYA imethibitisha kuwa Rais wa MAREKANI DONALD TRUMP amezungumza kwa njia ya simu na Rais UHURU KENYATTA juu ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi hizi mbili.

 

Taarifa inasema viongozi hao WAWILI wamejadili juu ya ushirikiano wa kiuchumi na ushirikiano wa pamoja katika kupambana na ugaidi na masuala mengine ya usalama katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

Rais TRUMP amesema ameutambua mchango wa KENYA katika kuchangia vikosi vya Umoja wa Afrika nchini SOMALIA na pia kujitolea kwa vikosi vya KENYA katika mapambano dhidi ya wanamgambo wa AL SHABAAB.

 

Viongozi hao pia wamezungumzia njia za kukuza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika KENYA na ukanda wa Afrika Mashariki kwa ujumla.

 

Rais UHURU KENYATTA amekuwa rais wa nne wa Afrika kuzungumza na rais huyo kutoka taifa lenye uwezo mkubwa duniani.

 

Marais wenige ambao wamezungumza na Rais DONALD TRUMP kwa njia ya simu ni Rais ABDEL FATAH AL SISI wa MISRI, Rais JACOB ZUMA wa AFRIKA KUSINI na Rais MUHAMMADU BUHARI wa NIGERIA.

 

 

GHANIA JUMBE

MACHI 08, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment