Responsive image
Responsive image
Posted : March 04, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Nasreen Karim (kushoto) akipitia kazi ya mwanafunzi Clare Musila wakati wa mafunzo hayo.
Responsive image

Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki  ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara,  mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa -CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ  tawi la Afrika Mashariki.

 

Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo  yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye  mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia  yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka  ya nchi zao wanazotoka.

 

Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria  na  mbinu tofauti za kupata ufadhili.

 

Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo  na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika.

 

Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding).

 

Mafunzo hayo ya  siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za  Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba  ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na  simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo.

 

Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika  ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo.

 

Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA)  unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la  kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki  ikiwemo Tanzania na Uganda.

 

Kwa sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo mengine ikiwemo Muziki na filamu.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment