Responsive image
Responsive image
Posted : February 28, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Responsive image

Serikali ya KENYA inatarajia kupiga marufuku matangazo ya serikali kutangazwa kwenye vyombo vya habari binafsi mara tu itakapozindua gazeti lake ambalo litasambazwa bure.

 

Hatua hiyo imekuja wakati Rais Uhuru Kenyatta anajiandaa kuzindua gazeti hilo la serikali ambalo litaandika habari kuhusu serikali ya nchi hiyo kwa usahihi zaidi na kuielimisha jamii jitihada zinazochukuliwa na serikali kuboresha maisha ya wananchi wake.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Matangazo la Serikali, magazeti yote nchini humo yanapata euro milioni 18 kwa mwaka kutokana na matangazo ya serikali.

 

Barua iliyotolewa naMkuu wa Utumishi wa Umma Kenya, Joseph Kinyua, imesema baraza la mawaziri limeidhinisha kuanzishwa kwa gazeti hilo la serikali litakaloitwa

 

Hata hivyo Shirika lisilo la serikali la kutetea uhuru wa kujieleza la limesema sera mpya ya serikali ya kupiga marufuku matangazo ya serikali katika vyombo vya habari nchini humo ni hatua ya kutaka kuthibiti vyombo vya habari binafsi nchini humo.

 

 

MARTHA NGWIRA

FEBRUARI 28, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment