Responsive image
Responsive image
Posted : February 27, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Kikosi cha usalama, BARINGO KENYA
Responsive image

Vikosi vya usalama nchini KENYA vimewekwa katika hali ya tahadhari Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo baada ya kuongezeka mauaji katika Kaunti ya BARINGO.

 

Msemaji wa Ikulu ya Rais MANOAH ESIPISU amewataka viongozi wa Kaunti ya BARINGO kuchukua hatua za kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo na kutoingilia hatua na shughuli za kibinadamu.

 

Amesema pia serikali haitawafumbia macho wanasiasa wanaowachochea watu kufanya machafuko.

 

Wakati huo huo Mashirika ya Kutetea Haki za Binadamu nchini KENYA yamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi JOSEPH BOINNET kupeleka vikosi zaidi katika Kaunti ya BARINGO baada ya wanasiasa wawili kuuawa.

 

Katika upande mwingine Baraza la Magavana limemtaka Rais UHURU KENYATTA kuchukua hatua za kurejesha amani na uthabiti katika kaunti hiyo.

        

Shirika la Msalaba Mwekundu la KENYA limetangaza kusimamisha shughuli zake za kibinadamu katika Kaunti ya BARINGO baada ya mfanyakazi wake kushambuliwa siku ya Ijumaa.

 

 

 

GHANIA JUMBE

FEBRUARI 27, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment