Responsive image
Responsive image
Posted : February 21, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Msemaji wa Rais wa KENYA, MANOA ESIPISU.
Responsive image

Serikali ya KENYA imeomba msaada wa mashirika ya kimataifa wa Dola zisizopungua Milioni 114 kwa ajili ya kukabiliana na athari za ukame ulioikumba nchi hiyo.

 

Kwa mujibu wa taarifa idadi ya watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula imeongezeka kutoka Milioni MOJA NA LAKI TATU mwezi Agosti mwaka jana na kufikia Milioni TATU mwezi Februari mwaka huu na kwamba kuendelea kwa ukame kumesababisha bei za bidhaa za vyakula kupanda kwa Asilimia 10 hadi 20.

 

Msemaji wa Rais wa KENYA, MANOA ESIPISU ametangaza kuwa hadi sasa serikali imetenga bajeti ya Dola Milioni SABINI NA TATU kwa ajili ya kukabiliana na athari za ukame ambapo Milioni 45 kati ya hizo zimetumika katika awamu ya kwanza ya mpango wa kukabiliana na baa hilo.

 

Katika ripoti yake Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu wa Misaada ya Kibinadamu imesema hali ya usalama wa chakula itakuwa mbaya zaidi katika nchi za SOMALIA, ETHIOPIA, ERITREA na KENYA.

 

 

GHANIA JUMBE

FEBRUARI 21,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment