Responsive image
Responsive image
Posted : February 17, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Silaha
Responsive image

Zaidi ya silaha ndogo ndogo na nyepesi LAKI TANO zimeingizwa nchini KENYA wakati nchi hiyo ikijitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka huu.

 

Silaha hizo ziko mikononi mwa jamii za wafugaji na kuleta wasiwasi ikiwa imebaki miezi MITANO kuelekea uchaguzi mkuu.

 

Vyombo vya usalama nchini KENYA vinafanya mikakati mbalimbali kutengeneza sheria ya kudhibiti na kuondoa uingizaji wa silaha nchini humo.

 

Afisa na mshauri wa kituo kinachofuatilia silaha ndogo ndogo na nyepesi KENYA na kanda ya Maziwa Makuu, FRANCIS WAIRAGU, amesema takwimu za kuwepo kwa silaha nyingi haramu nchini KENYA zinatia wasiwasi.

 

WAIRAGU amesema kuwa mara nyingi wakati vyombo vya usalama vinapoanza juhudi za kukamata silaha hizo haramu zilizopo mikononi mwa wananchi, kumekuwa na taarifa ya matumizi ya nguvu na vyombo vya dola kinyume cha sheria.

 

Wasiwasi huo unatokana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/8 ulioifanya KENYA kuongeza juhudi za kuwatia mbaroni ili  kupunguza umiliki wa silaha hizo.

 

 

JUDICA LOSAI

FEBRUARI 17, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment