Responsive image
Responsive image
Posted : May 17, 2018 (6 days ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa akizindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jijini Dar es Salaam
Responsive image

Rais Dkt. John Magufuli ametoa mwezi mmoja kwa wote wanaodaiwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania -JWTZ kulipa na kuagiza mara baada ya muda huo kupita vyombo vyote vya ulinzi na usalama viwatafute na kuwafikisha mbele ya sheria.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo Jijini DSM wakati wa uzinduzi wa kituo cha uwekezaji cha JWTZ kinachoratibiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) chini ya shirika lake la SUMA JKT pamoja na kuzindua kiwanda cha maji ya kunywa ya UHURU PEACK kinachomilikwa pia na JWTZ.

Awali Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu wameeleza jinsi walivyojipanga kuendeleza viwanda hivyo.

 

AGNES MBAPU

MEI 17, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment