Responsive image
Responsive image
Posted : May 16, 2018 (7 days ago) By TBC
Responsive image
Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Profesa Palamagamba Kabudi na Mkurugenzi wa Tanzanite One Faisal Juma wakitia saini makubaliano kuhusu utendaji wa kampuni ya Tanzanite One katika sekta ya madini
Responsive image

Kampuni ya madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa serikali fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na utendaji wake wa awali ulioitia hasara serikali.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema makubaliano hayo yametiwa saini jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati iliyoundwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Profesa Palamagamba Kabudi na  Mkurugenzi wa Tanzanite One Bw.Faisal Juma.

Prof. Kabudi amesema Tanzanite One imekubali kulipa fidia Serikali kutokana na mambo iliyofanya ambayo yalikuwa kinyume na utaratibu ulioleta hasara kwa serikali.

Amesema fidia hiyo inatakiwa kulipwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza italipwa ndani ya wiki mbili kuanzia leo Jumatano na haitahusisha Kodi. Pia Kampuni hiyo italazimika kulipa kodi na tozo nyingine zote zinazodaiwa na Serikali.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma amesema kampuni hiyo itahakikisha inafuata taratibu zote za Sheria ya Madini ya mwaka 2010 kwa lengo la kuhakikisha rasilimali ya madini inawanufaisha Watanzania na kwamba uvunjifu wa sheria uliofanywa na kampuni hiyo hautajirudia tena.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment