Responsive image
Responsive image
Posted : May 11, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Eneo lilikokumbwa na mafuriko; Picha na REUTERS
Responsive image

Waokoaji wameendelea na msako katika eneo lote lililopitiwa na mafuriko makubwa yaliyotokea baada ya kingo za bwawa liitwalo Patel kuvunjika Jumatano wiki hii, ili kuwapata walionusurika au kuupata miili ya waliokufa bila kupatikana, kama wapo.

Hadi leo Ijumaa idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko hayo imefikia 49 huku watu wengine kadhaa wakiripotiwa kuwa wamepotea.

Mafuriko yalitotokana na mvua kubwa zilizokuwa zinanyesha huko Kenya yalibomoa kuta za bwawa hilo linalomilikiwa na mtu binafsi huko Rifti Valley, kiasi cha kilomita 150 kaskazini mwa jiji la Nairobi na kuongeza maji kwenye mafuriko hayo kiasi cha kupelekea maafa karibu katika kijiji kizima.

"Eneo tunalotafuta manusura ni kubwa kuanzia kwenye bwawa lenyewe kuelekea chini kote” amesema Pius Masaai ambaye ni msemaji wa kitengo cha maafa cha taifa la Kenya.

"Pia tumefungua dawati maalum la kufuatilia taarifa za watu waliopotea kutoka kwenye familia zao” ameliambia shirika la habari la Al Jazeera.

Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya, ambalo kwa kushirikiana na vikosi vya uokoaji vya wilaya ya Nakura liliokoa watu 41 waliokuwa chini ya matope, Alhamisi, familia zipatazo 500 hazina makazi katika eneo la Solai na eneo pana la shamba la Nyakinyua.

"Familia hizi zinahitaji msaada wa muda mrefu wa serikali na wadau wengine wenye huruma” amesema Abbas Gullet katika taarifa yake kwa vyombo vya habari. Gullet ni Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya.

Imeripotiwa kuwa zaidi ya watu 20 waliokutwa wamekufa ni watoto. Ripota wa Al-jazeera Andrew Simon amesema “Hatuwezi kuonyesha baadhi ya picha ambazo tunazo hadi sasa, lakini watoto ambao ndio viumbe dhaifu kuliko wote kweye majanga kama haya, ndio wahanga wakubwa wa tukio hili”.

"Shuhuda mmoja aliyerejea katika eneo la tukio baada ya  mafuriko kupita amesema jirani yake ambaye alikuwa ni mlemavu wa macho alikufa baada ya maji kuvunja nyumba yake na kumzoa kwa vile hakuweza kukimbia.

 “Mwili wake ulipatikana asubuhi” amesema shuhuda huyo Veronica Wanjiku Ngigi  (67) na kuongeza kuwa majirani zake wengine wamekufa pia. “Nyumba zetu zote zimeharibiwa” amesema.

Bwawa la Patel lilijengwa ili kumwagilia maji shamba kuwa la maua linalomilikiwa na mfanyabiashara binafsi ambaye pamoja na maua pia huuza nje ya nchi kahawa, matunda na mazao mengine.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment