Responsive image
Responsive image
Posted : May 06, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Meneja wa zamani wa klabu ya Manchester United, Alex Ferguson
Responsive image

Meneja wa zamani wa timu ya Manchester United Alex Ferguson bado yuko chini ya uangalizi wa karibu wa wauguzi na madaktari baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura Jumamosi kutibu tatizo kwenye ubongo wake.

Taarifa ya uongozi wa Man United imesema upasuaji umefanyika vizuri lakini haikwenda mbali zaidi kuelezea  hali ya Ferguson (76) baada ya upasuaji huo.

Ferguson alistaafu umeneja wa Manchester United mnamo Mei 2013 baada ya kujipatia makombe 38 katika kipindi chake cha uongozi katika soka.

Familia ya Ferguson imeomba pawe na faragha wakati afya yake ikishughulikiwa katika hospitali ya Salford Royal.

"Tumemuweka Alex pamoja na familia yake katika fikra zetu katika kipindi hiki na tumeungana kumtakia apone haraka”, imesema taarifa iliyotolewa na Man United kupitia mtandao wa twitter.

“Anahitaji kukaa chini ya uangalizi maalum ili apone haraka” imeongeza taarifa hiyo.

Ferguson anatambulika kama meneja aliyekuwa na mafanikio makubwa kuliko wote katika historia ya soka la Uingereza.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment