Responsive image
Responsive image
Posted : April 25, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Matokeo ya mechi kati ya Serengeti Boys na timu ya vijana ya Kenya
Responsive image

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Serengeti Boys imefuzu hatua ya fainali katika mashindano ya ya CECAFA chini ya umri wa miaka 17, yanayofanyika Nchini Burundi.

Serengeti Boys wametinga fainali baada ya kuwalaza vijana wa Kenya mabao mawili kwa moja katika mchezo mgumu wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano hayo uliochezwa kwenye dimba la Muyinga .

Jafari Juma na Kelvin Paul ndio wameifungia Serengeti Boys mabao ya ushindi katika dakika za 21 na 62 , mabao yanayoipeleka Serengeti Boys katika hatua hiyo ya fainali.

Vijana hawa wanaonolewa na kocha Oscar Mirambo akiwa na mshauri wa benchi la ufundi Kim Paulsen sasa watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Uganda na Somalia katika hatua ya fainali.

Vijana wa Uganda na Somalia wanachuana katika nusu fainali ya pili kwenye dimba la Gitenga.

ENOCK BWIGANE

25 APRILI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment