Responsive image
Responsive image
Posted : April 23, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Jengo la Yanga
Responsive image

Yanga  imethibitisha rasmi kukata rufaa kwenye kamati ya saa 72  wakilalamikia matendo mawili kwenye mchezo wao wa jana dhidi ya Mbeya City uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Yanga inamlalamikia  mchezaji Eliud Ambokile ambae alifanyiwa mabadiliko lakini aliendelea kuwemo uwanjani na pia wanalalamikia kitendo cha mlinzi wa Mbeya City Ramadhan Malima aliyepewa kadi nyekundu kurudi uwanjani kushangilia goli pamoja na kuendelea kukaa kwenye benchi.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja huku Yanga wakitangulia kufunga kupitia kwa kiungo wake Raphael Daud na Mbeya City wakasawazisha kwenye dakika za majeruhi kupitia kwa Idd selemani maarufu kwa jina la Idd Nado.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment