Responsive image
Responsive image
Posted : April 25, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Kocha wa timu ya Simba, Pierre Lechantre
Responsive image

Wakati Yanga wakimtambulisha kocha wao mpya, habari zinaarifu kuwa Kocha wa timu ya Simba, Pierre  Lechantre amepeleka maombi ya kuifundisha timu ya Taifa ya Cameroon.

Kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Lechantre ni miongoni mwa makocha 77 waliotuma maombi kwa shirikisho la mpira wa miguu la Cameroon (Fekafoot) kuomba kazi hiyo ya ukocha. 

Jina la kocha Lechantre ni la tatu katika orodha ya majina hayo 77 ya makocha walioomba kazi hiyo ambapo makocha wengine ni pamoja na kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Raymond  Domeneh , Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Lota  Matteus, kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Wels, John Toshack , kocha wa sasa wa timu ya Taifa ya Iran, Carlos  Kuizeiro,  Nahodha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon, Rigobert Song na Nahodha na kocha wa zamani wa Timu ya Taifa ya Nigeria, Samson  Siasia.

Makocha hao wote majina yao yatachujwa na kubakia majina mat atu yatakayoitwa kwa ajili ya usaili wa mwisho na kisha kutangazwa kwa jina la kocha mpya wa timu ya Taifa ya Cameroon.

Makocha hao wanasaka kibarua cha kurithi mikoba ya kocha Hugo  Bruuz aliyeiongoza Cameroon kutwaa taji la mataifa ya Afrika mwaka 2017 na kujiunga na klabu ya Ostende ya Ubelgiji aambako amepewa majukumu ya Ukurugenzi wa ufundi.

ENOCK BWIGANE

25 APRILI 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment