Responsive image
Responsive image
Posted : April 25, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys
Responsive image

Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Serengeti Boys leo inashuka dimbani kuchuana na Kenya katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza katika mashindano ya CECAFA chini ya umri wa miaka 17, yanayofanyika nchini Burundi.

Mchezo huu unachezwa katika dimba la Muyinga ambapo kocha msaidizi wa Serengeti Boys, Oscar Milambo na kocha mkuu wa vijana wa Kenya, Mike Amenga, wametamba kuwaandaa vyema vijana wao kupata matokeo ya ushindi katika mchezo huo wa leo.

Nusu fainali ya pili inachezwa katika dimba la Gitenga ambapo vijana wa Uganda wanavaana na vijana wenzao wa Somalia.

MUNGU IBARIKI SERENGETI BOYS, MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 

ENOCK BWIGANE

25 APRILI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment