Responsive image
Responsive image
Posted : April 17, 2018 (7 days ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
Responsive image

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amemsimamisha kazi Meneja wa Kitengo cha Bahari na maeneo tengefu Dkt. Milali Machumu na kuvunja Bodi ya wadhamini ya Kitengo hicho.

Waziri Mpina ametoa uamuzi huo wakati akitoa ufafanuzi wa hoja zilizojitokeza kwenye taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), aliyowasilisha wiki iliyopita.

Moja ya maeneo yaliyotajwa kuwa na mapungufu ni usimamizi dhaifu wa rasilimali za bahari na maeneo tengefu ya bahari ambapo hoja zaidi ya 24 zilijitokeza katika eneo hilo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment