Responsive image
Responsive image
Posted : April 17, 2018 (7 days ago) By TBC
Responsive image
Maofisa wa polisi mkoani Pwani wakikagua athatri za mvua mkoani humo
Responsive image

Mvua zimeharibu miundombinu mkoani Pwani na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya vijijiji vya Mafizi na Gwata wilayani Kisarawe na makao makuu ya wilaya hiyo.

Akizungumzia athari za mvua kwa mkoa wa Pwani, Kamanda wa Polisi mkoa huo Jonathan Shana amesema mvua imeharibu miundombinu ya barabara ya Bagamoyo ikiwa ni pamoja na kuangusha nguzo za umeme.

 Amesema kwa sasa jeshi hilo kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto  wako katika tahadhari kubwa kuhakikisha wanakabiliana na madhara yoyote yatakayotokana na mvua hizo.

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Pwani wameomba serikali kuzuia watu kuweka makazi ama kufanya shughuli zozote katika maeneo ya mabondeni ili kuepusha maafa.

Mamlaka ya Hali ya Hewa imetoa tahadhari nyingine ya kuendelea kwa vipindi vya mvua kubwa katika mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Lindi na Mtwara pamoja na maeneo ya Zanzibar na kuwataka watu kuchukua tahadhari.

JOSEPH CHIWALE

APRILI 16, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment