Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
Responsive image

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema mkataba baina ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kampuni ya Star Media ulikuwa na kasoro zilizosababisha TBC kutopata gawio kwa miaka saba mfululizo.

Waziri Mwakyembe amesema hayo mjini Dodoma wakati akijibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG.

Waziri Mwakyembe amesema baada ya TBC kusaini mkataba wa maridhiano na Kampuni ya Star Media, Wizara yake itamchukulia hatua kali yeyote atakayeenda kinyume na makubaliano hayo.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema wizara yake inaandaa mkakati wa kukuza ujasiriamali utakaowezesha sekta hiyo kukua.

IDD MAALIM

APRILI 13, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment