Responsive image
Responsive image
Posted : April 14, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Jeshi la Syria
Responsive image

Serikali ya Syria imeyaita mashambulizi ya mataifa ya magharibi kwenye mitambo yake ya kijeshi, kuwa ya kikatili na kwamba yamekiuka sheria za kimataifa.

Marekani, Ufaransa na Uingereza zimefanya mfululizo wa mashambulizi ya angani Jumamosi asubuhi katika maeneo ya karibu na mji mkuu wa Damascus na katikati mwa mji wa Homs.

Operesheni hiyo ya pamoja imekuja wiki moja baada ya shambulizi la kemikali linalodaiwa kufanywa kwenye mji unaodhibitiwa na waasi nje kidogo ya Damascus na kuwaua watu 40. Mataifa ya magharibi yalimtuhumu rais Bashar al Assad kwa shambulizi hilo, lakini Syria na mshirika wake Urusi wamekana madai hayo na kuyatuhumu mataifa hayo kwa kutengeneza tukio hilo ili kuhalalisha hatua za kijeshi. 

Rais Donald Trump amesema Marekani  iko  tayari  kuendelea  na hatua dhidi ya  Assad  hadi  pale  atakapofikisha  mwisho  kile  rais  huyo alichosema  utaratibu  wake  wa  kihalifu wa  kuwauwa raia  wake kwa  silaha  za  sumu  zilizopigwa  marufuku  kimataifa. 

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment