Responsive image
Responsive image
Posted : April 13, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais wa Marekani Donald Trump
Responsive image

Rais wa Marekani Donald Trump amewatahadharisha askari wa Russia nchini Syria kuwa tayari wakati wowote jeshi la Marekani huenda likafyatua mabomu dhidi yao.

Kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twiter Trump amesema wamesikitishwa sana na vikosi vya Russia kuachia bomu la sumu katika mji wa Damascus nchini Syria na kusababisha vifo vya raia na uharibifu wa mali.

Trump amesema kwa sasa uhusiano wa Marekani na Russia sio mzuri na machafuko yatokeayo nchini Syria yanasababisha vita baridi kati yao ,huku Russia ikijua wazi kwamba bado inahitaji msaada wa kiuchumi kutoka taifa la Marekani.

Wakati huo huo televisheni ya serikali ya Russia imewatangazia wananchi kukufungasha vitu muhimu vitavyoweza kuwasaidia kwa muda mrefu iwapo watalazimika kuishi kwenye mahandaki kutokana na vita ya dunia ya 3 inayonukia.

Ukiacha vyakula na maji ya kutosha wananchi wameshauriwa kuwa na madini ya 'iodine' ambayo hulinda mwili dhidi ya sumu inayotokana na mionzi (radiation).  

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment