Responsive image
Responsive image
Posted : April 08, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva aliyeanza kutumikia kifungo cha miaka 12 jela
Responsive image

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ameanza rasmi kutumikia kifungo cha miaka 12 gerezani baada ya kukutwa na hatia za rushwa.

Lula da Silva amejisalimisha mwenyewe polisi leo baada ya kukwepa kwenda mahakamani na kujificha katika jengo la wafanyakazi wa chuma kwa kipindi cha siku mbili.

Lula mwenye umri wa miaka 72 alionekana akiingizwa kwenye magari ya polisi kutoka katika ofisi nyumbani kwake karibu na mji wa Sao Paulo.

Lula alikuwa akiwania uchaguzi wa urais we mwezi Oktoba, lakini kifungo chake kinaziacha wazi mbio hizo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment