Responsive image
Responsive image
Posted : April 08, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao ilipopambana na Wolaita Dicha ya Ethiopia
Responsive image

Kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa amesema ushindi wa bao mbili kwa bila dhidi ya Wolaita Dicha umewaweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Goli la mapema la Raphael Daud na goli la kipindi cha pili la Emmanuel Martin yalitosha kabisa kuipa Yanga ushindi huo wa bao mbili kwa bila.

Nahodha wa Yanga Nadir Haroub Canavaro anasema wamepambana ndio maana wamepata ushindi huo muhimu katika mchezo wa kwanza .

Mashabiki wa Yanga nao wamesema timu yao inanafasi kubwa ya kutinga hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Baada ya matokeo ya hayo Yanga sasa wanahitaji sare katika mchezo wa marudiano nchini Ethiopia ili kuweza kusonga mbele katika hatua ya makundi ya michuano hiyo ya kombe la shirikisho barani afrika, huku Dicha wakitakiwa kuwafunga yanga kuanzia mabao matatu kwa bila kama wanataka kusonga mbele.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment