Responsive image
Responsive image
Posted : April 04, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Marehemu Winnie Medikizela Mandela enzi za uhai wake.
Responsive image

Chama cha African National Congress (ANC) kinatarajiwa wakati wowote kutoa ratiba ya shughuli mbali mbali za kufanywa katika siku 10 zijazo kuhusiana na maombolezo ya kifo cha Mama Winnie Medikizela Mandela.  

Katibu Mkuu wa ANC Ace Magashule ameongoza ujumbe wa mawaziri na wajumbe wa Kamati Kuu ya ANC kutengeneza ratiba hiyo kwa kushirikiana na wanafamilia huko Soweto.

Msemaji wa ANC Pule Mabe amesema ratiba hiyo itawahusisha pia wasanii waliowahi kucheza nafasi kama Winnie Mandela katika filamu mbali mbali zilizokuwa zikielezea maisha yake.

Kitabu cha maombolezo pia kitafunguliwa nyumbani kwa wanafamilia lakini pia mitandaoni.

Mapema, Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini alisema shughuli za kuaga mwili wa Mama Winnie zitafanyika katika uwanja wa Orlando huko Soweto siku ya Jumamosi Aprili 14 mwaka huu na kwamba mwili wake utazikwa katika eneo la Fourways, Kaskazini mwa jiji la Johannesburg.

Kwa sasa bendera zote nchini Afrika Kusini na kwenye balozi zake ulimwenguni zimekuwa zikipepea nusu mlingoti hadi hapo mwili wa Winnie utapokuwa umezikwa. 

Rais Ramaphosa pia ameangaza siku 12 za maombolezo ya kitaifa.

 “Rais Ramaphosa amesema wazi kuwa Winnie Madikizela Mandela anastahili heshima ya kiwango cha juu kutokana na mchango wake katika ukombozi wa Afrika Kusini. Rais anaendelea kutuma salamu zake za rambi rambi kwa familia ya Mama Winnie akiwatakia ujasiri katika kipindi hiki kigumu kwao” amesema msemaji wa Rais Ramaphosa Khusela Diko.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment