Responsive image
Responsive image
Posted : April 05, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten
Responsive image

Mashabiki wa timu ya Yanga wametakiwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye mchezo wa timu yao wa hatua ya mtoano kuwania kufuzu kuingia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Africa dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia utakaochezwa siku ya Jumamosi kwenye dimba la Taifa.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten amesema mashabiki ni watu muhimu sana hivyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuishangilia timu yao mwanzo mwisho kwenye mchezo huo wa kombe la shirikisho barani Afrika.

Kwenye mchezo huo Yanga itawakosa wachezaji wake wanne kutokana na kuwa na kadi mbili za njano ambao ni Obrey Chirwa, Papy Kabamba , Juma Said na mlinzi mkongwe Kelvin Yondani.

Yanga imeangukia kwenye kombe la shirikisho baada ya kutolewa  katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na timu ya Township Rollers ya Botswana.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment