Responsive image
Responsive image
Posted : March 18, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Eneo ambapo baadhi ya miili ya watu waliouawa katika mauaji ya Rwanda imezikwa
Responsive image

Nchi za Afrika zimeshauriwa kujifunza kutokana na mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 kama sehemu muhimu ya kulinda amani iliyopo katika nchi zao ili kuepuka kutumbukia katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.

Ushauri huo umetolewa na Wakuu wa Umoja wa Vyombo vya Utangazaji Barani Afrika (AUB) katika eneo la Gisozi yalipo makaburi ya pamoja ya zaidi ya watu 250,000 waliouawa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Rwanda zaidi ya miaka 24 iliyopita.

Kwa sasa jumba hili la makumbusho ya mauaji ya kimbari limekuwa darasa kwa raia wa mataifa mengine kuja kujifunza chanzo na athari ya kupoteza amani ili yaliyotokea nchini Rwanda yasije kuwakuta na wao.

Kutokana na somo la mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda sasa nchi hiyo imeendelea kushikamana na kujenga umoja miongoni mwa wananchi jambo ambalo limesaidia kupiga hatua kubwa ya maendeleo baada ya kufungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza kitendo kinachofanya uchumi wa taifa la Rwanda kunawiriki kwa kasi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

 

GABRIEL ZAKARIA

MACHI 18, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment