Responsive image
Responsive image
Posted : March 18, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Wachezaji wa Simba na Yanga wakati wa kombe la Mapinduzi mwaka huu
Responsive image

Baada bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga kutupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kushuka katika kombe la shirikisho barani Afrika ikisubiri mechi za kapu, mchezo wake wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya hasimu wake Simba sasa utapigwa kalenda.

Yanga walilazimishwa suluhu dhidi ya wenyeji Township Rollers ya Botswana hapo jana na hivyo kuondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa kwa kipigo cha jumla cha mabao mawili kwa moja na sasa wanaangukia katika kombe la shirikisho ambapo michezo yake ya mchujo kusaka tiketi ya hatua ya makundi zitaanza kuchezwa April 6 na 7 na marudiano itakuwa baada ya siku kumi.

Kwa mujibu wa ratiba ya ligi kuu Tanzania bara Simba na Yanga wamepangwa kukutana Aprili 7 katika mchezo wa mzunguko wa pili ambapo Simba watakuwa wenyeji.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment