Responsive image
Responsive image
Posted : March 07, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Rais Kim Jong – Un wa Korea Kaskazini
Responsive image

Viongozi wa Korea  Kaskazini na Korea Kusini wanatarajiwa kufanya mkutano mwezi ujao, kwa mujibu wa Korea Kusini.  Huo utakuwa ni mkutano wa kwanza wa aina hiyo kwa zaidi ya miaka 10 na wa kwanza tangu Kim Jong –Un alipoingia madarakani nchini Korea Kaskazini.

Ujumbe huo pia umeongeza kuwa Kim amesema angependa kuzungumza kuhusu kuachana na silaha za nyuklia ikiwa tu atahakikishiwa usalama wa nchi yake.  Kim na Rais wa Korea Kusini  Moon-Jae-In watakutana kwenye mpaka wenye ulinzi mkali mwezi ujao katika kijiji cha mapatano cha Pan Munjon

Aidha maofisa wa Korea Kusini wamesema Kim amewaambia  kuwa hakutakuwa na majaribio ya makombora wakati mazungumzo yakiendelea.

Kwa upande wake, Marekani imesema mazungumzo kati yake na Korea Kaskazini yatafanyika ikiwa tu nchi hiyo itakuwa tayari kuzungumzia suala la kuondoa silaha za nyuklia.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment