Responsive image
Responsive image
Posted : January 27, 2018 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Responsive image

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza watu anaopendekeza waidhinishwe kuwa mawaziri katika serikali yake mpya baada yake kushinda uchaguzi mwaka jana, huku mawaziri sita ambao walikuwa wanahudumu katika serikali yake muhula uliopita wakibadilishiwa kazi na kuteuliwa kuwa mabalozi.

Walioteuliwa kuwa mabalozi ni pamoja na Dan Kazungu, aliyekuwa waziri wa madini, ambaye sasa amependekezwa kuwa balozi mpya wa Kenya nchini Tanzania.

Kazungu anajaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa balozi wa Kenya nchini Tanzania Chirau Ali Mwakwere kujiuzulu mwaka jana ili kuwania kiti cha ugavana katika uchaguzi uliofanyika Agosti 8, 2017.  

Hivi karibuni Tanzania imefanya mabadiliko makubwa katika mifumo ya sheria, kanuni na uendeshaji wa biashara ya madini kwa ujumla ili kuiwezesha sekta hiyo iliyokuwa na mianya mingi ya wizi, kuwa na mchango mkubwa zaidi katika pato la taifa.

Wachambuzi kutoka nchi nyingi za Afrika wamepongeza harakati hizo za kulinda raslimali za taifa, zinazoongozwa na Rais John Magufuli.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment