Responsive image
Responsive image
Posted : December 29, 2017 (4 months ago) By TBC
Responsive image
Rais mteule wa Liberia George Weah
Responsive image

Rais mteule wa Liberia George Weah ameahidi kufanya mabadiliko kadhaa ya kuleta maendeleo nchini humo na kuahidi kushirikina na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi hiyo ili kufanikisha azma hiyo.

Weah ambaye anakuwa mwanasoka wa kwanza ulimwenguni kuchaguliwa kuwa Rais wa nchi, amesema hayo baada ya kutangazwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa mzunguko wa pili ambapo ameibuka na ushindi wa zaidi ya asilimia 60 ya kura zilizopigwa huku mpinzani wake ambaye ni makamu wa Rais wa sasa wa Liberia Joseph Boakai akipata asilimia 38 ya kura hizo.

Kufuatia ushindi huo, wafuasi wa George Weah wamejitokeza katika mitaa ya jiji la Monrovia kupongeza ushindi huo ambapo baadhi yao wamesema wana imani na Rais huyo mteule katika kuboresha mambo mbalimbali nchini humo.

Waangalizi wa uchaguzi huo kutoka ndani na nje ya nchi hiyo wamesema uchaguzi ulikuwa huru na haki ambapo mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi huo yaliboreshwa ikilinganishwa na uchaguzi wa awali uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Katika uchaguzi huo wa awali Weah alipata ushindi wa asilimia 38 huku mpinzani wake Boakai akipata ushindi wa asilimia 28 na hivyo kurudiwa kwa uchaguzi, ndipo Weah akaibuka  na ushindi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment