Responsive image
Responsive image
Posted : November 14, 2017 (3 months ago) By TBC
Responsive image
Msemaji wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR, WILLIAM SPINDLER
Responsive image

Umoja wa Mataifa umeanza zoezi la kuwahamisha wakimbizi wa nchi za Afrika walioko LIBYA na kuwapeleka nchini NIGER.

 

Msemaji wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa-UNHCR, WILLIAM SPINDLER amesema wakimbizi hao ambao walikuwa katika hali mbaya ya kibinadamu wamehamishwa kutoka LIBYA hadi NIGER ili kunusuru maisha yao.

 

Amesema hao ni raia kutoka nchi za ERITREA, ETHIOPIA na SUDAN na watabaki NIGER hadi mchakato wa kuwarejesha katika nchi zao utakapokamilika.

 

Zaidi ya wahamiaji Eltu TATU miongoni mwao wamepoteza maisha kwa kuzama baharini au kufa kwa njaa na kiu jangwani wakisubiri kusafirishwa.

 

 

GHANIYA JUMBE

13 NOEMBA 2017.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment