Responsive image
Responsive image
Posted : September 18, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Mshambuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi
Responsive image

Mzunguko wa tatu wa ligi kuu soka Tanzania bara umemalizika kwa kuchezwa michezo miwili siku ya jumapili ambapo Simba walikuwa wenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga kwenye uwanja wa Uhuru huku Mbeya City wakiwakaribisha Njombe Mji katika dimba la sokoine.

Nyota wa Kiganda Emmanuel Okwi amefunga magoli mawili kwenye ushindi wa bao tatu kwa bila waliopata Simba dhidi ya Mwadui FC na kupanda hadi kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Okwi amefunga goli la kwanza kwenye dakika ya saba ya mchezo huo kwa shuti la nje ya kumi na nane na akaongeza  goli la pili  kwenye kipindi cha pili katika dakika ya 67 na goli la tatu lilitiwa kimiani na John Bocco (Adebayo) kwenye dakika ya 72 ya mchezo huo na  kuifanya Simba iendelee kuwa na mtokeo mazuri  kwenye msimu huu.

Hadi sasa Simba imefikisha alama saba huku ikiwa imefunga magoli kumi na nyavu zake zikiwa hazijatikishwa hata mara moja ikiwa imecheza michezo mitatu na mshambuliaji wake Emmanuel OKwi anaongoza kwenye orodha ya wafungaji akiwa amefunga magoli sita.

Kwa upande wake John Bocco goli alilofunga ni goli lake la kwanza kuifungia timu hiyo ya Msimbani tangu ajiunge nayo kwenye msimu huu akitokea Azam FC ambayo aliichezea kwa karibu muongo mmoja.

Katika mchezo mwingine Mbeya City imepata ushindi mwembamba wa goli moja kwa bila dhidi ya timu ya Njombe Mji ambayo hadi sasa haina alama hata moja baada ya kupoteza michezo yake yote mitatu.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies Fashionmalula masanja  |  4 months ago   |   December 07, 2017
"axante xana wanamcmbaz"

Leave Your Comment