Responsive image
Responsive image
Posted : September 14, 2017 (5 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Donald Trump wa Marekani
Responsive image

Rais Donald Trump wa Marekani na baadhi ya wabunge wa chama cha Republican wametangaza mpango wao wa kuwalinda watu wanaoitwa waota ndoto au watoto wa wahamiaji waliozaliwa nchini Marekani.

 

Wanasiasa hao wamesema wanatafuta njia za kuwalinda watoto wa wakimbizi halisi, ambao walizaliwa nchini humo na hakuna nchi nyingine wanayoijua isipokuwa nchi ya Marekani.

 

Wanasiasa hao wa Marekani wanaelekea kukubaliana na sera ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama, ya kuwalinda watoto wa wakimbizi.

 

Viongozi mbalimbali wa kidini nchini Marekani wamekuwa wakiendesha ibada maalumu ya kuwaombea watu hao iliyokuwa ikiambatana na taratibu za kuwaosha miguu.

 

Utaratibu wa kuoshana miguu makanisani umekuwa ukifanywa kwa ukumbusho wa kifo cha Yesu Kristo na ishara ya kuonyesha upendo na mshikamano kwa watu wote.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment