Responsive image
Responsive image
Posted : September 14, 2017 (7 months ago) By TBC
Responsive image
Mchezaji Paul Pogba wa Manchester United
Responsive image

Mchezaji Paul Pogba wa Manchester United huenda akakosekana kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kuumia nyama za paja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ambao timu yake iliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya timu ya FC BASEL.

 

Mchezaji huyo raia wa Ufaransa mwenye miaka 24 ameafanyiwa vipimo siku ya jumatano ili kujua ukubwa wa tatizo lake lakini taarifa za awali zinaonyesha atakuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha yake kwa mwezi mmoja na wiki sita.

 

Kutokana na majeraha hayo Pogba atazikosa mechi ambazo timu yake itacheza dhidi ya Everton, Southampton na Crystal Palace kwenye ligi kuu, pia atakosa mechi ya kombe la ligi dhidi ya Burton FC na mechi ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya CSKA Moscow.

 

Lakini pia nyota huyo atakosa mechi za kufuzu kombe la dunia litakalofanyika nchini Russia mwaka 2018 ambapo timu yake ya taifa itacheza na Bulgaria na Belarus.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment