Responsive image
Responsive image
Posted : August 28, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Yanga yashindwa kabisa kupata goli la ushindi dhidi ya Wanapaluhengo. katika msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara
Responsive image

 

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Yanga wameanza msimu mpya kwa kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja na timu iliyopanda daraja msimu huu Lipuli FC ya mkoani Iringa maarufu kwa jina la Wanapaluhengo.

Mshambuliaji Seif Karihe aliifungia Lipuli FC goli la kuongoza kwenye dakika ya 44 ya mchezo huo kabla ya Donald Dombo Ngoma kuisawazishia Yanga kwa kufunga goli kwa kichwa .

Pamoja na kuliandama lango la Lipuli kwa muda mwingi Yanga walishindwa kabisa kupata goli la ushindi huku mlinzi na nahodha wa Lipuli FC , Mghana, Asante Kwesi akilimwa kadi nyekundu kwenye dakika za mwisho kabisa za mchezo huo na kufanya timu yake imalize ikiwa na wachezaji pungufu.

 

Evance Mhando

Agosti  2​8​, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment