Responsive image
Responsive image
Posted : July 21, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
wasanii Ambwene Yesaya maarufu kama AY na Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA
Responsive image

Mahakama kuu ya Tanzania imetupilia mbali  rufaa iliyofunguliwa  na kampuni ya Tigo kupinga kuwalipa  wasanii Ambwene Yesaya maarufu kama AY na Hamis Mwinjuma  maarufu kama Mwana FA kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni mbili kwa kutumia nyimbo zao bila kulipa.

Wakili Alberto Msando ambaye amewawakilisha wasanii hao amesema  kwamba huo ni ushindi muhimu kwa sanaa  ya Tanzania.

Amesema  wasanii hao ni haki yao kulipwa kwa sababu  kazi zao zinalindwa kisheria.

Wasanii hao walishinda kesi yao ya madai ambapo  waliishtaki kampuni ya TIGO kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu kwa ajili ya wateja wao pasipo makubaliano.

 

Angella Msangi

Julai 21,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionAthuman Mtinda  |  7 months ago   |   September 14, 2017
"Ongezeni juhudi"

Leave Your Comment