Responsive image
Responsive image
Posted : June 19, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Responsive image

Watu wawili wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kushambulia hoteli moja ya kitalii nchini Mali na kuanza kuwashambuli watalii waliokuwa katika eneo hilo.

Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyoko nchini Mali, yalifika katika eneo hilo la kitalii, lililoko karibu na mji wa Bamako na kufanikiwa kuwaokoa watalii 36 waliokuwa wakishikiliwa mateka na watu hao wenye silaha.

Waziri wa ulinzi wa Mali amesema mmoja kati ya watu waliohusika na tukio hilo amefanikiwa kutoroka akiwa na majeraha pia Serikali ya Mali imesema tukio hilo ni la kigaidi.

 

 

Nyambona Masamba

Juni 19,2017

==

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment