Responsive image
Responsive image
Posted : June 10, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Askari wa Umoja wa Mataifa nchini Mali.
Responsive image

Umoja wa Mataifa umelaani vikali kuuawa askari wake wa kulinda amani nchini Mali na kutoa wito wa kukomeshwa vitendo hivyo.

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kitendo cha makundi ya wapiganaji kuwaua askari hao ni kosa la jinai.

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametaka wale wote waliohusika na jinai hiyo kupandishwa kizimbani na sheria kufuata mkondo wake.

 

Aidha ameongeza kuwa vitendo vya wanamgambo wa Mali vya kuwaua askari wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali havikubaliki hata kidogo na vinapaswa kukomeshwa.

 

Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa hapo jana ilieleza kuwa, wanamgambo wenye silaha siku ya Alkhamisi waliwashambulia askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nje ya kambi yao katika Mji wa KIDAL kaskazini mwa nchi hiyo.

 

Askari watatu wa kikosi hicho cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Mali -Minusma waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment