Responsive image
Responsive image
Posted : May 18, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake, kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Responsive image

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Makamu wa Rais Mama Samia ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake, kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama  askari wanaume katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema anaimani kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment