Responsive image
Responsive image
Posted : May 18, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage
Responsive image

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema serikali inatekeleza mkakati wake wa kuiwezesha sekta binafsi kuchangia maendeleo na ukuaji wa viwanda nchini.

Akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018 bungeni mjini Dodoma,  Waziri Mwijage  amesema sekta binafsi ina mchango mkubwa katika kufanikisha azma kuwa na Taifa lenye maendeleo ya viwanda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Stanslaus Nyongo amesema katika suala la kufufua na kukuza viwanda lazima sekta ya nishati ya umeme ipewe kipaumbele.

Katika mwaka wa Fedha wa 2017/2018 Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeomba kupatiwa zaidi ya Shilingi  Bilioni 122 ikiwa ni zaidi kwa asilimia 49.2  ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017.

 

 

MARIA KAPARASULA

MEI 18, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment