Responsive image
Responsive image
Posted : May 18, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha wa timu ya Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino
Responsive image

Kocha wa timu ya Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amesema atabakia kwenye timu hiyo  na kukanusha taarifa kuwa anaweza kuununua mkataba wake ili aweze kuondoka kwenye timu hiyo.

Muargentina huyo amekuwa kocha wa Tottenham tangu mwaka 2014 alipojiunga nayo akitokea Southampton na kusainia kandarasi ya miaka mitano na mwezi mei mwaka jana akaongeza kandarasi ya kubakia hadi mwaka 2021.

Mwenyewe Pochettino amekiri kwa kusema kumekuwa na fununu nyingi za yeye kuondoka ila anawakikishia hawezi kuondoka na hakuna sababu ya yeye kuondoka.

Kocha huyo amekuwa akihusishwa na kujiunga na Barcelona ambayo kocha wake ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu ila pamoja na kukutana na Rais wa timu hiyo amesema itakuwa ngumu mno kwake kujiunga na miamba hiyo ya Hispania.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment