Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo
Responsive image

Waziri wa Nishati na Madini  Prof. Sospeter Muhongo ameiagiza bodi mpya ya wakala wa umeme vijijini REA kuhakikisha maeneo  yote ya visiwa vilivyopo kwenye bahari na maziwa, yanafikiwa na nishati ya umeme wa jua ndani ya  kipindi cha miaka miwili.

Prof. Muhongo amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wananchi wenye fursa ya kutumia umeme vijijini ukilinganisha na idadi ya sasa ya asilimia 49.5.

Pia Prof. Muhongo ameitaka bodi hiyo  kujiridhisha na uwezo wa wakandarasi wanaopatiwa zabuni kazi hapa nchini.

Aidha serikali inaendelea na mikakati endelevu ya kuhakikisha inatimiza ahadi yake ya kufikisha huduma ya nishati ya umeme vijijini  kama inavyozungumza kwenye ilani ya Chama Cha Mapinduzi.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment