Maisha ya Steve Biko
Natumai u-bukheri wa afya msomaji wa tovuti ya Habari na Muziki ya TBC Taifa, karibu ukaribie katika makala ya TAMBUA, hii ni makala inayotilia maanani zaidi jambo moja ambalo wengi hawalifahamu, Kwa juma hili TAMBUA inasafiri na kufanya maskani yake ya muda nchini Afrika Kusini, kunako jimbo la Eastern Cape, hapa tunatuama na kuyaangazia maisha ya STEPHEN BANTU BIKO, almaarufu STEVE BIKO
STEPHEN BANTU BIKO
Huyu alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu hususani, mtu mweusi, akikabiliana kwa ujasiri mkubwa na ubaguzi wa rangi nchini humo, ubaguzi wa rangi kwa kipindi kirefu cha ukoloni nchini Afrika ya Kusini ulimweka mtu mweusi katika daraja ya chini kabisa, daraja la mwisho ambalo kwa namna nyingine halikuwa tofauti na wanyama wa mwitu waliojongea kwa miguu minne.

Disemba 18, 1946, Steve Biko anazaliwa katika eneo la Tylden katika jimbo la Mashariki (Hivi sasa likijulikana kama Jimbo la Mashariki la Cape), alikuwa mmoja ya watoto watano kwa baba Mzingaye Biko na mama Nokuzola Macethe Duna.

Baba yake Mzee Mzingaye kwa muda fulani hivi alikuwa askari polisi, na baadae akawa Karani katika Ofisi ya Mambo ya Ndani ya Mji wa King William. Katika kiwango cha kati cha elimu, alijiandikisha katika Chuo Kikuu cha Afrika ya Kusini (UNISA) akifanya masomo kwa njia ya posta, mzee huyu hakufikia ndoto zake kwani alifariki kabla ya kupata Shahada yake ya Kwanza ya Sheria.

Hatimae familia hii ikahamia rasmi katika mji wa King William, Mashariki mwa Cape, na baadae huko Ginsberg mnamo mwaka 1948, eneo ambalo lilitengwa maalum kwa watu weusi waliokuwa mjini King William, na akina Biko wakajipatia nyumba yao katika mtaa wa Zaula.

Mzee Mzingaye Biko alifariki dunia ghafla mwaka 1950, Steve alikuwa na miaka minne, yeye na nduguze wakabaki katika malezi ya mama yao aliyewalea akitegemea kibarua chake kama mpishi kunako hospitali ya Grey

Unaweza kuzisikiliza makala hizo hapo chini
Mwandishi:   |   Essero Mafuru
Mhariri:   |   Batlet Milanzi
 
JAN 18, 2016
JAN 19, 2016
JAN 20, 2016
MOST POPULAR NEWS