
NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dakt. ASHA ROSE MIGORO ameendelea na ziara yake hapa nchini ambapo hii leo pamoja na shughuli nyingine amekuwa na mazungumzo na Mkuu wa Majeshi Jenerali DEVIS MWAMUNYANGE.
Akiwa ofisini kwa Mkuu wa majeshi, Dakt. ASHA ROSE MIGIRO amesema umoja wa mataifa una imani kubwa na Jeshi la wananchi wa TANZANIA na unatoa wito kwa jeshi hilo kuendelea kujitayarisha na kuongeza ushiriki wake katika ulinzi wa amani.
Naibu Katibu Mkuu huyo pia ametumia fursa hiyo, kulipongeza jeshi la wananchi wa TANZANIA kwa jinsi linavyotekeleza majukumu yake na kusema kuwa Umoja wa Mataifa haujapata taarifa yoyote ya dosari kuhusu vikundi vinavyolinda amani.
Kwa upande wake, Jenerali MWAMUNYANGE amemhakikisha Dkt. MIGIRO kuwa JWTZ linawashirikisha wanajeshi wa kike wengi zaidi kulingana na mahitaji
Ziara ya DKT ASHA ROSE MIGIRO katika ofisi na taasisi hapa nchini inalenga kudumisha uhusiano uliopo katika Umoja na Mataifa na nchi mbalimbali.



